
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKUNGUNI."
May 7, 2026 - 30"
Radio and PodcastLive Radio & Podcasts
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya ku...
08 MEI 2026 is an episode from Habari za UN by UN Global Communications (Digital Solutions Unit). Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo...
This episode belongs to Habari za UN.
Use the player on this page to stream the episode online.
Published May 8, 2026, 10:55 long, audio available.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bado watu wana kumbukumbu mbichi za ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema wanaendelea kuratibu na kufuatilia kwa karibu mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea kwenye meli ya kifahari ya kitalii na kwamba “Hatari ni ndogo kabisa, hii si COVID mpya.”Matthew Hollingworth ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) amerejea hii leo kutoka Somalia na kuwaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi yale aliyojionea akiwa ziarani nchini humo kwa wiki moja kuwa “ Nimeona familia ambazo zimeshuhudia madhara mengi kwa wakati mmoja ikiwemo athari za hali mbaya ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi, athari zote hizo zimekuwa zikisukuma njaa hadi katika viwango vya hatari .”Na, Wanawake na wasichana nchini Lebanon wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kukimbia makazi yao licha ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa Aprili 17 mwaka huu, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
You can listen to 08 MEI 2026 online on Radio and Podcast. Open the player on this page to stream the available audio.
08 MEI 2026 is an episode from Habari za UN by UN Global Communications (Digital Solutions Unit).
This episode is 10:55 long.
This episode was published on May 8, 2026.
Yes. Use the heart button on the episode page to add it to your favorite episodes list.
Yes. This page shows related episodes from Habari za UN when more episodes are available from the podcast feed.
You can listen to 08 MEI 2026 on this page when the episode audio is available from the podcast feed.
08 MEI 2026 is from Habari za UN by UN Global Communications (Digital Solutions Unit).
Published May 8, 2026 and 10:55 long